#CECAFAU17: Serengeti boys yachezea shilingi chooni.

Michuano ya Cecafa chini ya umbri wa miaka kumi  na saba (17) idjumapili hiyi imeingia katika siku yake ya pili huku Tanzania ikitoka sare ya bao moja kwa moja (1-1) dhidi ya Uganda mchezo uliopigwa  mkoani Muyinga katika uwanja wa Umuco.

Vijana wa Serengeti boys ndio walio tangulia kuzifumania nyavu za wapinzania wao dadika ya ishirini (20’) ya kipindi cha kwanza kupitia moja mwa washambuliaji wao mahiri sana anae utumia mguu wa kusoto, Jafari Juma Mtoo, jezi nambari tisa (9) mgongoni ikawa ni furaha kwa kocha wao mdenmark huyu, Kim Poulsen.

Serengeti boys walicheza vizuri kipi  cha kwanza cha mchezo, walitawala uwanja hadi kufikia mapunziko walikua wakiongoza kwa bao moja kwa sufuri (1-0).

Kipindi cha pili mambo yaliwageukia na kuturuhusu kutumia ulie msemo wa kiswahili kua kutumbua cha mtoto akiishi mchanga, Tanzania iliwaruhusu waganda kipindi cha pili kucheza hususani pale walipokua Serengeti boys wakijilaza uwanjani wakijua kwamba wana poteza mdaa kumbe wakajikokotea bala ndipo dakika ya 40’ ya kipindi cha pili waganda wakasawazisha kupitia Jaggwe Musa nakufanya kocha wake Onen Peter awe mwenye tabasamu, kusawazishiwa bao huko kwa vijana wa Tanzania kulimfanya kocha wao mdermark Kim Poulsen kuondoka kwenye benchi la ufundi na kuamua kuingia katika vyumba vya kuvalia kabla ya dakika 5’ mchezo umalizike.

Mchezo huyo ambao ulikua ukichezeshwa na refa kutoka Somalia, Mohamed Nur na wasaidizi wake mmoja kutoka Kenya, Oliver Omondi pamoja na Hassan Mao msomalia, mchezo ulimalizika dakika 90’ timu zote zikitoshana nguvu ya bao moja kwa moja.

Michezo mingine ambayo alichezwa hiyi idjumapili nikwamba tu, Ethiopia waliirarua Somalia bao tatu kwa moja (3-1) katika mchezo uliopigwa kule mkoani ngozi katika uwanja wa urukundo.

Katika mchezo ambao ulikua ukisubiriwa kwa hamu kubwa kule mkoani gitega katika uwanja wa Ingoma kati ya Zanzibar na Sudan haukuchezwa kutokana na sababu za miaka ya wachezaji wa Sudan ambayo inadhanikua kua ni mingi kiasi.

Fahamuni kwamba michezo hiyo ya Cecafa under 17 yatarajia kuendelea hiyi idjuma inne.

 

Ismail (Nahodha) Kwizera

Ismail (Nahodha) KWIZERA ni mwandishi habari za Spoti, Uhusiano, na Burudani kwenye Journal Magara Times. Bwana KWIZERA pia ni mtangazaji wa vipindi vya Spoti kwenye Radio Magara Times FM. Wasiliana na Ismail kwenye: ismailk@magaratimes.com

0 Comments

No comments!

There are no comments yet, but you can be first to comment this article.

Leave reply

Only registered users can comment.