#CECAFAU17:BURUNDI yaanza mashindano vibaya wakati wao niwenyeji

 Michuano ya kombe la Cecafa kwa timu za taifa kutoka ukanda wa afrika mashariki kwa wale vijana wasio zidisha umbri wa miaka kumi na saba (17 ) yameanza kutimua vumbi hiyi idjuma mosi kule mkoa Muyinga kwenye uwanja wa Umuco.

Kwenye mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa mashindano hayo ya Cecafa under 17, wenyeji Intamba mu Rugamba (Burundi) hawakua na lao mbele ya timu ya Harambe Stars (Kenya),ambapo Intamba mu rugamba imeshuhudia mabao ma 4 kwa nunge, yakiingia katika wavu wake, Vijana wa Kenya wamefanikiwa kipindi cha kwanza cha mchezo huyo kufunga mabao ma wili (2), nahivyo kipindi cha pili Kenya wakaja kumalizia kazi ambayo walikua tayari wameshaifanya kwenye kipindi cha kwanza  nakuongeza  mabao mengine ma wili (2) kipindi cha pili nakuwaacha wenyeji wakiwa hoyi mbele ya mashabiki zao.

Harambe stars,vijana hao wa Kenya tayari wamesha jiandikishi poenti zao tatu (3) za kwanza kwenye kundi A, lenye timu kama Burundi wenyeji, Somalia na Ethiopia.

Wachezaji walio anzishwa kenye mchezo huyu waleo

Kwa upande wa Intamba mu Rugamba ya wadogo ni:

HABUKA Papy, MOSI Djuma, IRUTINGABO Faustin, MASUMBUKO Jules, NDIKUMANA Ally, BUKURU Samir,

IRATANGA Flavier, NIYONDIKO Davy Chastel, NIBIKORA Arthur, MUNABA Edson, NIKUZE Guy Chris.

Walikua wakiongozwa na mwalimu Vivier BAHATI.

Kwa upande wa Kenya ama Harambe stars ya wadogo

Walianzisha hawa wafuatao:

BRIAN Opiyo OLONGO, Hillary ODHIAMBO, Christophe RAILA, Telvin MAINA Heijkers, Costah Anjeo Nzuva, Saidi Musa KAONEKA, Arnold ONYANGO, Movine Otiendo OMONDI, Felix CHABAYA, Mathew MWENDA.

Walikua wakiongozwa na mwalimu Chris AMINO.

Michuano hiyo inatarajia kuendelea hiyi idjumapipi,

Ambapo kutatarajiwa kuchezwa michezo mi tatu (3) kwenye saa moja ya 15H30 kwenye viwanja tofauti,

Somalia VS Ethiopia mkoani Ngozi uwanja wa Urukundo.

Sudan VS Zanzibar mkoani Gitega uwanja wa Ingoma.

Uganda VS Tanzania mkoani Muyinga uwanja wa Umuco.

Fahamuni kua hiyi ni mara ya pili kwa taifa la Burundi kupokea michuano ya Cecafa yawa vijana hao wasio zidisha umbri wa miaka 17, mara ya kwanza ilikua ni 2006 ambapo kombe lilibaki inchini humo.

About Ismail (Nahodha) Kwizera

Ismail (Nahodha) KWIZERA ni mwandishi habari za Spoti, Uhusiano, na Burudani kwenye Journal Magara Times. Bwana KWIZERA pia ni mtangazaji wa vipindi vya Spoti kwenye Radio Magara Times FM. Wasiliana na Ismail kwenye: ismailk@magaratimes.com

Check Also

Watu saba wafariki  kwa ugonjwa kipindupindu Haiti

#VOA. | Watu saba wafariki kwa ugonjwa kipindupindu Haiti

Haiti siku ya Jumapili imesema takriban watu saba wamefariki dunia kwa ugonjwa kipindupindu katika kurudi …

RDC : la Monusco note une amlioration de la situation des droits humains entre juin et septembre | Politico.cd

#PoliticoCD. | RDC : la Monusco note une amlioration de la situation des droits humains entre juin et septembre | Politico.cd

Dans un rapport adress au Conseil de Scurit de lONU, la Monusco note une nette …