Inter Stars: Timu 2 vigogo za haba inchini Burundi tayari zimesha anza kumkodolea macho HAKIZIMANA Hamimu.

Vital'o FC na LLBS4A zimesha anza kumsaka chipukizi alie chaguliwa kama mchezaji bora mwenye umbri mdogo wa Primus Ligue

                               Kuanzia kulia Mabano Shaban, Hakizimana Hamim na Ismail Kwizera

Kiugo mshambuliaji wa timu ya Inter Stars, HAKIZIMANA Hamimu almaarufu “Hafidh”alie chaguliwa kama chipukizi bora wa mwaka kwenye ligi la Primus Ligue tayari amesha anza kukodolewa macho na vilabu bi wili vigogo hapa inchini Burundi licha ya timu yake ya Inter Stars kushuka daraja.

HAKIZIMANA Hamimu katika mahojiano na Magaratimes  ya hapo jana katika fukwe za bahari maeneo ya Zion Beach palipokua panatolewa tunzo mbali mbali kwa wachezaji n’awalimu bora walio fanya vizuri kwenye ligi la Primus Ligue msimo ulio malizika alilieleza gazeti hili kua timu za Lydia Ludic Sport 4Africa na Vital’o FC ni miongoni mwa vilabu ambavyo vimeanza kumyatia kijana huyo.

Hamimu alifunguka na kusema pale tulipokua tuna muuliza kua je kuna timu zozote ambazo zimeanza kujitokeza kwa kukusaka? Alijibu na kusema kua “tayari kuna timu mbili zimesha anza kunitafuta” tukamuuliza pia kua kama sio siri timu hizo  ni zipi? Alijibu hivi “Ni Vital’o FC na LLBS4A”.

Hakizimana Hamimu aliwutoa pia ushauri kwa wavijana wenye rika kama lake akiwaomba kuendelea wanasikiliza ushauri na kukazana na vipaji vyao ipo siku watayaona matunda kama yake na akahitimisha kabisa nakusema kua mchezaji ambae anae mpenda wa bara la ulaya ni Marco Asensio wa Real Madrid.

Ismail (Nahodha) Kwizera

Ismail (Nahodha) KWIZERA ni mwandishi habari za Spoti, Uhusiano, na Burudani kwenye Journal Magara Times. Bwana KWIZERA pia ni mtangazaji wa vipindi vya Spoti kwenye Radio Magara Times FM. Wasiliana na Ismail kwenye: ismailk@magaratimes.com

0 Comments

No comments!

There are no comments yet, but you can be first to comment this article.

Leave reply

Only registered users can comment.