#Burundi #CANU23: Intamba Murugamba U-23 Yailaza Kilimanjaro Warriors Mjini Bujumbura.

kipindi cha pili ndipo mabao yalipoanza kupatikana kupitia penalty ilio fungwa na mshambuliaji wa Rayon Sports inchini Rwanda, Bimenyimana Bonfils Caleb baada ya mabeki wa Kilimanjaro Warriors kuunawa mpira kwenye eno lahatari na bao lapili lilipachikwa na Cedrick Titi Mavugo ambae aliekuwa ametokea benchi kuichukua nafasi ya Caleb akaipachika timu yake bao la pili kwa kichwa.

Timu ya taifa ya Burundi chini ya umbri wa myaka 23, Intamba murugamba wamefanikiwa kuilaza Tanzania ya vijana chini ya umbri huyo maarufu Kilimanjaro Warriors kwaushindi mnono wa bao mbili bila (2-0), Katika mchezo wa kwanza wa kuisaka tiketi ya kuelekea Masri 2019, kwenye kombe la mataifa barani Afrika chini ya umbri wa myaka 23 ulio pigwa mjini Bujumbura katika uwanja wa mwanamfalme Louis Rwagasore.

Kilimanjaro Warriors mazowezini katika uwanja wa Mwanamfalme Louis Rwagasore.

Kipindi cha kwanza cha mchezo huyo kimemalizika timu zote zikitoshana nguvu ya bila bila (0-0), baadae katika kipindi cha pili ndipo mabao yalipoanza kupatikana kupitia penalty ilio fungwa na mshambuliaji wa Rayon Sports inchini Rwanda, Bimenyimana Bonfils Caleb baada ya mabeki wa Kilimanjaro Warriors kuunawa mpira kwenye eno lahatari na bao lapili lilipachikwa na Cedrick Titi Mavugo ambae aliekuwa ametokea benchi kuichukua nafasi ya Caleb akaipachika timu yake bao la pili kwa kichwa. Dakika tisini zikamalizika, inne zikaongezwa mechi ikamalizika Burundi U-23 wakitoka kifua mbele kwa mabao hayo 2-0 dhidi ya Tanzania U-23.

Mchezo wamarudi utapigwa tarehe 20 Novemba 2018 kule Dar Es Salaam, Tanzania U-23 watakua wenyeji dhidi ya  Burundi U-23

Ismail (Nahodha) Kwizera

Ismail (Nahodha) KWIZERA ni mwandishi habari za Spoti, Uhusiano, na Burudani kwenye Journal Magara Times. Bwana KWIZERA pia ni mtangazaji wa vipindi vya Spoti kwenye Radio Magara Times FM. Wasiliana na Ismail kwenye: ismailk@magaratimes.com

0 Comments

No comments!

There are no comments yet, but you can be first to comment this article.

Leave reply

Only registered users can comment.