#VOA. | Mwinyi amteua Masoud kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar

PUBLICITÉS:

Marehemu Seif Sharif Hamad

Marehemu Seif Sharif Hamad

Hatua hiyo imekuja baada ya chama cha ACT Wazalendo kukamilisha mchakato wa kupendekeza jina la atakaye rithi nafasi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar, Zena Said imesema Rais Mwinyi amezingatia kifungu cha 9(3) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Tamko la serikali ya Zanzibar

Tamko la serikali ya Zanzibar

Kifungu hicho kinasema, ‘Muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar utakuwa wa Umoja wa Kitaifa na utendaji wa kazi zake utafanywa katika utaratibu utakaohakikisha kuendelezwa kwa umoja nchini na kutimiza lengo la kufikia demokrasia.’

Pia Rais wa Zanzibar, Mwinyi amepewa uwezo chini ya kifungu Namba 39(3) cha Katiba ya Zanzibar kufanya uteuzi huo.

“Baada ya kushauriana na Chama cha ACT-Wazalendo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Hussein Mwinyi amemteua Mheshimiwa Othman Masoud Othman Sharif kuwa Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar,” imesema taarifa hiyo.

Kulingana na taarifa hiyo uteuzi huo unaanza Machi Mosi na sherehe za kumwapisha Masoud zitafanyika Jumanne Machi 2 katika ukumbi wa Ikulu ya Zanzibar.

Masoud amewahi kuhudumu katika nafasi za ngazi za juu katika serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwemo mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwa sasa ni mwanachama wa ACT Wazalendo.

Kadhalika anatambuliwa kwa msimamo wake usioyumba wa kutetea maslahi ya Zanzibar ndani na nje ya nchi na pia uwezo wake mkubwa kwenye taaluma yake ya sheria.

Source link: Habari hii imetoka kwenye wavuti wa VOA Swahili.

PUBLICITÉS:

 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
Habari za VOA

VOA - SAUTI YA AMERIKA: ni wakala wa media wa Merika ambao hutumika kama taasisi ya serikali ya Merika kwa utangazaji usio wa kijeshi, wa nje. Ni mtangazaji mkubwa zaidi wa kimataifa wa Merika. VOA inazalisha vitu vya dijiti, TV na redio katika lugha 47 ambazo husambaza kwa vituo vya ushirika kote ulimwenguni.

0 Comments

No comments!

There are no comments yet, but you can be first to comment this article.

Leave reply

Only registered users can comment.