Primus League: Matokeo na msimamo wiki ya 25 ya ligi kuu Burundi.

Wiki ya 25 ya ligi kuu inchini Burundi maarufu Primus, ni kwamba timu ya askari Polisi Rukinzo FC ambayo ipo katika mbio za kuwania  ubingwa iliishinda timu ya Olympic Star  kutoka mkoani Muyinga mabao  (2-1). Inter Star ilishindwa dhidi ya Kayanza United nyumbani katika uwanja wa Intwari mjini Bujumbura  mabao (0-2). Messager Ngozi FC nyumbani katika uwanja wa Urukundo,  waliishinda bila tabu timu ya Royal FC mabao (2-0).  Musongati FC ikiwa nyumba mkoani Gitega katika uwanja wa  Ingoma waliishinda Aigle Noir CS bao  (1-0) na kuiweka kileleni timu hiyo ya mjii mkuu wa kisiasa.  Flambeau Du Centre imekua ugenini dhidi ya Athletico Academy katika uwanja wa Intwari mjini Bujumbura mambo hayakua mazuri kwa upande wao maana walishindwa dhidi ya Athletico Academy mabao (3-1). Kushindwa huko kwa Flambeau Du Centre kumewatoa na fasi ya kwanza. Mabao yote hayo matatu ya Athletico Academy yamefungwa  na Alexis Kitenge mshambuliaji wa zamani wa AFC Leopards ya Kenya.

Timu ya Musongati FC ikiwa katika uwanja wa Ingoma mkoani Gitega.

Wiki hii ya 25 inatarajiwa kutamatika hii ijumatatu ambapo, timu ya Bujumbura City wataipo Vital’O FC majira ya  alasiri katika uwanja wa Intwari mjini Bujumbura.

Haya hapa matokeo ya wiki hiyo ya 25.

BS Dynamic 0-2 Bumamuru FC

Muzinga FC 2-1 Les Eléphants FC

Inter Star 0-2 Kayanza United

Rukinzo FC 2-1 Olympic Star

Messager Ngozi FC 2-0 Royal FC

Musongati FC 1-0 Aigle Noir CS

Athletico Academy 3-1 Flambeau Du Centre.

Msimamo wa muda wa wiki ya 25.

1. Musongati FC alama 46 (goli 18)

2. Messager Ngozi FC 46pts  (+13)

3. Rukinzo FC 46pts (+12)

4. Flambeau Du Centre 45pts (+15)

5. Kayanza United 43pts (+6)

6. Aigle Noir CS 40pts (+10)

7. Olympic Star 36pts (+5)

8. Royal FC 34pts (+3)

9. Vital’O FC 34pts (0) (-1 mchezo mmoja pungufu)

10. BS Dynamic 32pts (-5)

11. Atletico Academy 31pts (-6)

12. Buja City 30pts (-4) (-1 mchezo mmoja pungufu)

13. Inter Star 28pts (-7)

14. Bumamuru FC 26pts (-13)

15. Les Eléphants FC 24pts (-14)

16. Muzinga FC 10pts (-30)

About Ismail (Nahodha) Kwizera

Ismail (Nahodha) KWIZERA ni mwandishi habari za Spoti, Uhusiano, na Burudani kwenye Journal Magara Times. Bwana KWIZERA pia ni mtangazaji wa vipindi vya Spoti kwenye Radio Magara Times FM. Wasiliana na Ismail kwenye: ismailk@magaratimes.com

Check Also

Watu saba wafariki  kwa ugonjwa kipindupindu Haiti

#VOA. | Watu saba wafariki kwa ugonjwa kipindupindu Haiti

Haiti siku ya Jumapili imesema takriban watu saba wamefariki dunia kwa ugonjwa kipindupindu katika kurudi …

RDC : la Monusco note une amlioration de la situation des droits humains entre juin et septembre | Politico.cd

#PoliticoCD. | RDC : la Monusco note une amlioration de la situation des droits humains entre juin et septembre | Politico.cd

Dans un rapport adress au Conseil de Scurit de lONU, la Monusco note une nette …