Musongati FC : Rukundo Jean De Dieu amekabidhiwa tunzo lake.

Mwalimu wa timu ya Musongati FC ya mkoa wa Gitega, alikabidhiwa tunzo lake la BCM Burundi kama mwalimu bora wa mwezi februari katika ligi kuu Burundi Primus League. Ilikua hiyi ijumapili katika uwanja wa Ingoma mkoani Gitega, kabla ya kuishinda Aigle Noir CS (1-0).

Mwalimu wa timu ya Musongati upande wa kuliya akiwa na viongozi wa Club BCM Burundi katika uwanja wa Ingoma mkoani Gitega.

Hiyi ni mara ya pili mfululizo kwa mwalimu Rukundo Jean De Dieu kutunzwa tunzo hilo. Mwalimu huyo wa zamani wa timu ya Kayanza United amekabidhiwa laki moja sarafu za Burundi (100.000fbu), bando yenye picha yake pamoja na tuzo.

Tuzo hilo la BCM Burundi ((Best Coach Of The Month Burundi) linatolewa kila mwezi kwa mwalimu anae fanya vizuri kuliko wengine kwenye ligi kuu Burundi. Linatolewa na wapenzi wa soka inchini Burundi walio jiunga na kuunda  Club BCM Burundi.

About Ismail (Nahodha) Kwizera

Ismail (Nahodha) KWIZERA ni mwandishi habari za Spoti, Uhusiano, na Burudani kwenye Journal Magara Times. Bwana KWIZERA pia ni mtangazaji wa vipindi vya Spoti kwenye Radio Magara Times FM. Wasiliana na Ismail kwenye: ismailk@magaratimes.com

Check Also

Watu saba wafariki  kwa ugonjwa kipindupindu Haiti

#VOA. | Watu saba wafariki kwa ugonjwa kipindupindu Haiti

Haiti siku ya Jumapili imesema takriban watu saba wamefariki dunia kwa ugonjwa kipindupindu katika kurudi …

RDC : la Monusco note une amlioration de la situation des droits humains entre juin et septembre | Politico.cd

#PoliticoCD. | RDC : la Monusco note une amlioration de la situation des droits humains entre juin et septembre | Politico.cd

Dans un rapport adress au Conseil de Scurit de lONU, la Monusco note une nette …