Ligue B: Timu ipi kati ya New Oil FC na Les Crocos FC itakayo zishindikiza timu za Top Junior na Flambeau de l’est ligi kuu ?

Timu ya  New Oil FC  kutokea mkoani Muyinga itachuana na timu ya Les Crocos FC kutokea mkoani Rumonge kwenye mchezo wa mchujo wakiisaka tiketi moja inayo saliya ya kushiriki ligi kuu Burundi maarufu kama Primus League msimo wa 2021-2022.  Mchezo huyo utachezwa hapo kesho ijumapili april 18/2021 majira ya alasiri  (15h00) saa za Burundi katika uwanja wa Umuco mkoani Muyinga, mashariki kaskazini mwa Burundi. Na mchezo wa marudio utachezwa april 28/2021 katika uwanja wa Intwari mjini Bujumbura mida ya alasiri.  Uwongozi wa Les Crocos FC ndio ulio amua mchezo huyo wa marudio uchezwe katika uwanja wa Intwari  tofauti na uwanja wa nyumbani wa Ivyizigiro mkoani Rumonge  ambao Les Crocos FC wamekua wakipokelea mechi zao.

Timu ya New Oil FC katika uwanja wa Umuco mkoani Muinga.

Ili timu hizo zijikute katika mchezo wa mchujo ni kutokana kwamba zilimaliza ligi zikishikilia na fasi ya pili katika msimamo wa  ligi daraja la pili (Ligue B) katika makundi ma wili ya timu nane nane. Fahamuni ya kwamba timu za Top Junior kutokea mkoani Kayanza pamoja na timu ya Flambeau de l’Est kutokea mkoani Ruyigi ndizo zimekwisha jipatia tiketi rasmi ya kushiriki msimo ujao ligi kuu Primus League baada ya kumaliza ligi daraja la pili zikishikilia na fasi ya kwanza kila timu katika kundi lake.  

Timu ya Les Crocos ikiwa katika uwanja wa Ivyizigiro mkoani Rumonge.

Tuwakumbushe kwamba timu tatu kutoka ligi daraja la pili Ligue B, ndizo zinazo panda daraja na kuelekea ligi kuu Primus League, kisha nyingine timu tatu zinashuka kutoka ligi kuu kuelekea daraja la pili. Timu ya Ngozi City na Agasaka Academy timu mbili kutokea Ngozi ndizo ambazo zilishuka kutoka daraja la pili na kuelekea daraja la tatu. 

About Ismail (Nahodha) Kwizera

Ismail (Nahodha) KWIZERA ni mwandishi habari za Spoti, Uhusiano, na Burudani kwenye Journal Magara Times. Bwana KWIZERA pia ni mtangazaji wa vipindi vya Spoti kwenye Radio Magara Times FM. Wasiliana na Ismail kwenye: ismailk@magaratimes.com

Check Also

Watu saba wafariki  kwa ugonjwa kipindupindu Haiti

#VOA. | Watu saba wafariki kwa ugonjwa kipindupindu Haiti

Haiti siku ya Jumapili imesema takriban watu saba wamefariki dunia kwa ugonjwa kipindupindu katika kurudi …

RDC : la Monusco note une amlioration de la situation des droits humains entre juin et septembre | Politico.cd

#PoliticoCD. | RDC : la Monusco note une amlioration de la situation des droits humains entre juin et septembre | Politico.cd

Dans un rapport adress au Conseil de Scurit de lONU, la Monusco note une nette …