Ligue B : Les Crocos FC yaweka mguu mmoja ndani ya Primus League.

Katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kutafuta tiketi ya kushiriki ligi kuu msimo ujao, ulio chezwa hiyi ijumapili ya wiki ilio malizika katika uwanja wa Umuco mkoani Muyinga,  timu ya New Oil FC walipotezea nyumani kwa kuchapwa bao moja bila (0-1) dhidi ya timu ya Les Crocos FC kutoka mkoani Rumonge. Ushindi huo wa kwanza wa Les Crocos FC umeyifanya timu hiyo kuzika mguu mmoja ndani ya ligi kuu Burundi kwa kusubiri mchezo wa marudio unao tarajiwa kuchezwa hiyi ijuma april 23 2021 katika uwanja wa Intwari mjini Bujumbura kunako majira ya alasiri (15h00).

Katika mchezo huyo wa marudio, vijana wa Gustave Niyonkuru (Les Crocos FC) wanahitaji kutoa sare ao kushinda mchezo ili kupanda daraja. Timu ya New Oil FC inayo funzwa na Nahimana Hussein « Welo », inalazimika kushinda (2-0, 2-1, 3-1, 3-2) ili ipate tiketi ya kushiriki ligi kuu msimo ujao. Ikiwa kama itashinda (1-0)  wata jibwaga kwenye mikwaju ya manati maana matokeo kwa ujumbla yatakua ni (1-1).

Ikumbukwe tu kwamba timu za Top Junior kutoka mkoani Kayanza na timu ya Flambeau De l’Est kutoka mkoani Ruyigi zimekwisha pata tiketi ya kushiriki ligi kuu Primus League  msimo ujao.

About Ismail (Nahodha) Kwizera

Ismail (Nahodha) KWIZERA ni mwandishi habari za Spoti, Uhusiano, na Burudani kwenye Journal Magara Times. Bwana KWIZERA pia ni mtangazaji wa vipindi vya Spoti kwenye Radio Magara Times FM. Wasiliana na Ismail kwenye: ismailk@magaratimes.com

Check Also

Watu saba wafariki  kwa ugonjwa kipindupindu Haiti

#VOA. | Watu saba wafariki kwa ugonjwa kipindupindu Haiti

Haiti siku ya Jumapili imesema takriban watu saba wamefariki dunia kwa ugonjwa kipindupindu katika kurudi …

RDC : la Monusco note une amlioration de la situation des droits humains entre juin et septembre | Politico.cd

#PoliticoCD. | RDC : la Monusco note une amlioration de la situation des droits humains entre juin et septembre | Politico.cd

Dans un rapport adress au Conseil de Scurit de lONU, la Monusco note une nette …