#ParsToday. | Balouji: Kuzusha tuhuma za uongo dhidi ya Iran ni mbinu ya kudumu ya wazayuni

PUBLICITÉS:

Mshauri wa ofisi ya uwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema, kuzusha tuhuma bandia na za uongo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ni mbinu ya kudumu inayotumiwa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ili kuficha na kuhafifisha uhalifu na jinai zake dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.

Heidar Ali Balouji, ameyasema hayo katika kikao cha Kamati ya Kwanza ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wakati akijibu porojo na tuhuma zisizo na msingi zilizotolewa na mwakilishi wa kizayuni dhidi ya Iran.

Balouji amesisitiza kuwa, hakuna uongo wala uzushaji mgogoro wowote bandia utakaoanzishwa na utawala wa Kizayuni ambao utaweza kuficha mbele ya walimwengu utambulisho na sura halisi ya uhalifu, ushupaliaji vita na uchu wa kujipanua ulionao utawala huo haramu; na akaongezea kwa kusema, Israel inakiuka waziwazi sheria za kimataifa, inakaidi kutekeleza maazimio ya Umoja wa Mataifa na inakiuka haki za msingi za watu wa Palestina.

Ukatili na unyama wanaofanyiwa hata watoto Wapalestina na askari wa Israel

Mshauri wa ofisi ya uwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema, Israel inafanya kila njia ili kutaka kuonyesha kuwa uwezo wa kijeshi unaokubalika kimataifa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mpango wake wa nyuklia ulio chini ya usimamizi kamili wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki ni changamoto kwa uthabiti wa eneo la Asia Magharibi; na akabainisha kwamba, hiyo ni hatua ya kinafiki na kizandiki ya kuzibabaisha fikra za waliowengi juu ya hatari halisi dhidi ya uthabiti wa eneo, hususan maghala ya silaha za nyuklia na vituo vingine vya nyuklia vya utawala huo ambavyo havifanyiwi ukaguzi wowote wa kimataifa…/ 

Source link: Habari hii imetoka kwenye watuti wa ParsToday.

PUBLICITÉS:

 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
ParsToday Kiswahili

0 Comments

No comments!

There are no comments yet, but you can be first to comment this article.

Leave reply

Only registered users can comment.