Ethiopia yavionya vyombo vya habari vya kimataifa

#VOA. | Ethiopia yavionya vyombo vya habari vya kimataifa

Mamlaka ya Habari ya Serikali Kuu ya Jamhuri ya Ethiopia imetuma barua ya onyo kwa mashirika ya habari ya Associated Press (AP), Reuters, CNN na shirika la utangazaji la BBC kwa kusambaza habari zinazochochea uadui kati ya watu na kuhujumu uhuru wa nchi hiyo.

Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Habari nchini humo Mohammed Edris Mohammed Ijumaa alituma barua za onyo kwa vyombo hivyo vya habari akidai kuwa mar akwa mara ripoti zao zimeegemea upande wa kikundi kinachoeneza ghasia nchini.

“Tangu kuanza kwa operesheni za vyombo vya dola katika Mkoa wa Kaskazini mwa Ethiopia kwa kusimamiwa na serikali Kuu, Mamlaka ya Habari Ethiopia imekuwa ikifuatilia vyombo mbalimbali vya habari vya kigeni na kufanya uchambuzi wa yanayovuma katika mwenendo wao wa ripoti zao juu ya suala hilo.

Bahati mbaya, mamlaka imegundua kuwa vyombo hivyo vya habari vilivyotajwa hapa juu vimeendelea kuandaa na kusambaza uchambuzi wa uongo wa habari juu ya Ethiopia ikisaidia malengo ya kikundi cha TPLF,” imesema sehemu ya onyo hilo kwa vyombo vya habari lililotolewa na Mohammed.

Mohammed ameongeza “Mamlaka ya Habari Ethiopia, katika kutoa leseni kwa shughuli za wanahabari inatarajia ripoti zao zisihatarishe maslahi ya kitaifa ya Ethiopia.”

Mamlaka hiyo ya vyombo vya habari imedai kuwa vyombo hivyo vinne vya habari katika ofisi za Afrika Mashariki vimeendelea kuripoti kuwa operesheni za vyombo vya usalama ni kampeni ya mauaji ya kimbari na hivyo kuzorotesha juhudi za serikali katika kutatua mgogoro wa kibinadamu unaoendelea katika mkoa wa Tigray.

Chanzo cha habarI hii ni Gazeti la ‘The East African’

Source link: Habari hii imetoka kwenye wavuti wa VOA Swahili.

 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  

About Habari za VOA

VOA - SAUTI YA AMERIKA: ni wakala wa media wa Merika ambao hutumika kama taasisi ya serikali ya Merika kwa utangazaji usio wa kijeshi, wa nje. Ni mtangazaji mkubwa zaidi wa kimataifa wa Merika. VOA inazalisha vitu vya dijiti, TV na redio katika lugha 47 ambazo husambaza kwa vituo vya ushirika kote ulimwenguni.

Check Also

Marche bloc patriotique : Gentiny Ngobila donne son aval et dtermine deux itinraires | Politico.cd

#PoliticoCD. | Marche bloc patriotique : Gentiny Ngobila donne son aval et dtermine deux itinraires | Politico.cd

– Publicit- Aprs la sance de travail qu’il a eu ce vendredi 26 novembre 2021 …

DRC: Waziri wa Utalii anashutumu usimamizi usio wazi wa Hifadhi ya Virunga na kujaribu kuinyakua na Fondati

#ActualiteCD. | DRC: Waziri wa Utalii anashutumu usimamizi usio wazi wa Hifadhi ya Virunga na kujaribu kuinyakua na Fondati

Waziri wa Utalii, Modero Nsimba, hana ulimi mfukoni. Anataka kuona waziwazi katika usimamizi wa mbuga …