UN yapitisha azimio dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel

#ParsToday. | UN yapitisha azimio dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel

PUBLICITÉS:

Umoja wa Mataifa umepitisha azimio linalosisitiza kuwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel hauna haki ya kupora rasilimali za watu wa Palestina na za miinuko ya Golan ya Syria unayoikalia kwa mabavu.

Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa (ECOSOC) limepitisha rasimu ya azimio iliyowasilishwa kwa ushirikiano wa Pakistan,- kwa niaba ya kundi la 77, ambalo ni shirika kubwa zaidi la kiserikali la nchi zinazoendelea wanachama wa Umoja wa Mataifa,- na China; azimio ambalo linabainisha maafa ya kiuchumi na kijamii yanayosababishwa na ukaliaji ardhi kwa mabavu wa utawala wa Kizayuni kwa hali za maisha za Wapalestina katika ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu ukiwemo mji wa Baitul Muqaddas (Jerusalem) na pia wakazi wa miinuko ya Golan inayokaliwa kwa mabavu.

Azimio hilo limepitishwa kwa kura 43 zilizounga mkono na kura nne zilizopinga huku nchi nne zikiamua kutopiga kura.

Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa

Azimio la Baraza la Kiuchumi na Kijamii la UN limetilia mkazo msingi wa mamlaka ya kudumu ya kumiliki maliasili zao mataifa yaliyovamiwa na ardhi zao kukaliwa kwa mabavu na likabainisha kwamba, kuna wasiwasi kuwa utawala wa Kizayuni unahatarisha na kuangamiza rasilimali za watu wa Palestina na za miinuko ya Golan ya Syria unayoikalia kwa mabavu.

Vilevile azimio hilo limesisitizia haki isiyokubalika kuporwa ya miinuko inayokaliwa kwa mabavu ya Golan na ya watu wa Palestina ya kutumia na kunufaika na rasilimali zao zote za maliasili na za kiuchumi…/  

Source link: Habari hii imetoka kwenye watuti wa ParsToday.

PUBLICITÉS:

About ParsToday Kiswahili

Check Also

Raisi: Njama za maadui za kuitenga Iran zimefeli

#ParsToday. | Raisi: Njama za maadui za kuitenga Iran zimefeli

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia njama za karibuni za maadui za kutaka …

Alkhamisi tarehe 29 Septemba 2022

#ParsToday. | Alkhamisi tarehe 29 Septemba 2022

Leo ni Alkhamisi tarehe Pili Rabiul Awwal 1444 Hijria sawa na tarehe 29 Septemba 2022. …