Mapigano baina ya Taliban na ISIS nchini Afghanistan wakati wa Muharram

#ParsToday. | Mapigano baina ya Taliban na ISIS nchini Afghanistan wakati wa Muharram

PUBLICITÉS:

Serikali ya kundi la Taliban nchini Afghanistan imetangaza kuangamizwa magaidi watatu wa genge la ukufurishaji la Daesh (ISIS) katika mapigano yaliyotokea kwenye eneo la Karte-Ye-Sakhi mjini Kabul.

Msemaji wa kundi la Taliban amesema kuwa mapigano yaliyotokea kwenye eneo hilo la Karte-Ye-Sakhi katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, yalianza siku ya Jumatano na magaidi wanne wa Daesh wameuawa na mwengine mmoja ametiwa mbaroni.

Zabiullah Mujahid ameongeza kuwa, magaidi hao walikuwa na nia ya kufanya vitendo vya uhalifu na mashambulizi ya kigaidi katika eneo hilo la Karte-Ye-Sakhi mjini Kabul ambalo siku hizi za Muharram limeshamiri maombolezo ya kuuawa shahidi Imam Husain AS, mjukuu wa Bwana Mtume Muhammad SAW katika jangwa la Karbala la Iraq ya leo mwaka 61 Hijria. 

Kimsingi mji wa Kabul ndio unaopaswa kuwa na usalama zaidi ikilinganishwa na miji na mikoa mingine ya nje ya mji mkuu huo wa Afghanistan. Sasa kutokea mapigano ndani ya mji huo baina ya askari wa Taliban na magaidi wa ISIS ni ishara kuwa genge hilo la kigaidi limejipenyeza katika maeneo nyeti na hassas na huenda hata ndani ya serikali ya Taliban. 

Waislamu wa eneo la Karte-Sakhi mjini Kabul Afghanistan katika maandilizi wa Tasua na Ashura

 

Ijapokuwa usalama ulitarajiwa kuimarika nchini Afghanistan kwa kuingia madarakani kundi la Taliban mwezi Agosti 2021, lakini matukio ya mwaka mmoja uliopita yanaonesha kuwa kundi hilo halijakabiliana vilivyo na magaidi wa Daesh.

Katika siku za awali za kurejea madarakani kundi la Taliban na baada ya kuipindua serikali ya Rais Muhammad Ashraf Ghani, kundi hilo liliahidi kwamba litaleta usalama na amani kwa kaumu, makabila, makundi na maeneo yote ya Afghanistan na itapambana vikali na magenge yote yanayochezea usalama na roho za wananchi wa Afghanistan.

Hata hivyo matukio ya mwaka mmoja uliopita huko Afghanistan yanaonesha kuwa utulivu na usalama wa kutia matumaini haujapatikana nchini humo. Genge la ukufurishaji la ISIS ni miongoni mwa magenge makubwa yanayofanya mashambulio ya mara kwa mara ya kigaidi katika maeneo na mikoa tofauti ya Afghanistan ukiwemo mji mkuu Kabul.

Ijapokuwa msemaji wa Taliban amesema kwamba mapigano hayo na magaidi wa Daesh yalifanyika kama sehemu ya siasa za kundi hilo za kuwadhaminia usalama Waislamu wa Kishia wanaoomboleza mauaji ya kikatili ya Imam Husain AS, lakini miezi iliyopita, magaidi wa ISIS walifanya mashambulio mengi ya kutisha na ya kinyama dhidi ya Waislamu wa Kishia waliokuwa kwenye ibada ya Sala Msikitini na kuua shahidi na kujeruhi mamia ya Waislamu hao.

Kwa kutilia maana uzoefu mchungu wa huko nyuma wa kushambuliwa na kuuliwa kigaidi na kinyama Waislamu wanaomboleza mauaji ya Imam Husain AS nchini Afghanista katika siku za Tasua na Ashura, linalotarajiwa kutoka kwa kundi la Taliban ni kuwa na ratiba makini na madhubuti mno ya kulinda usalama wa waombolezaji wa Imam Husain AS katika mwezi huu wa Muharram, hususan katika siku hizi nyeti na muhimu mno za Tasua na Ashura.

Eneo ambalo Waislamu wa Afghanistan hukusanyika kwa wingi katika maombolezo ya Imam Husain AS hasa siku za Tasua na Ashura

 

Bahram Zahedi ni mtaalamu wa masuala ya eneo hili. Kuhusu malengo ya mashambulizi ya genge la Daesh nchini Afghanistan anasema:

Moja ya shabaha na malengo ya Daesh (ISIS) nchini Afghanistan ni kuzusha mifarakano na mizozo katika jamii ya nchi hiyo hususan baina ya Waislamu wa Kishia na Kisuni. Hadi hivi sasa lakini wameshindwa kufanya hivyo. Mifano iko wazi. Moja ya mifano hiyo ni shambulizi la mabomu lililofanywa na Daesh ndani ya Msikiti wa Mashia mjini Kandahar kwa lengo la kuzusha chuki na mzozo baina ya Masuni na Mashia, lakini kwa bahati nzuri hali ilikuwa kinyume kabisa na walivyotarajia magaidi wa ISIS kwani safu ndefu za Waislamu wa Kisuni zilionekana Kandahar kuwapa pole Waislamu wenzao wa Kishia. Hali iliyojitokeza baada ya shambulio hilo la kigaidi ilikuwa ya udugu na mapenzi makubwa katika safu za Waislamu wa madhehebu yote kiasi ambacho hakijapata kushuhudiwa nchini Afghanistan.

Shambulizi la hivi karibuni la genge la kigaidi la ISIS katika maabadi ya Wahindu nchini Afghanistan, ni ushahidi mwingine unaothibitisha kwamba lengo hasa la magaidi wa Daesh ni kuzusha vita vikubwa vya kidini na kimadhehebu nchini humo. Serikali ya Taliban ambayo ndiyo iliyoko madarakani hivi sasa, ina jukumu la kuhakikisha wananchi wote wa Afghanistan wanaishia kwa usalama na amani bila ya kujali uchache wa kaumu na makabila yao na bila ya kuangalia wako kwenye mikoa na sehemu gani?

Source link: Habari hii imetoka kwenye watuti wa ParsToday.

PUBLICITÉS:

About ParsToday Kiswahili

Check Also

Raisi: Njama za maadui za kuitenga Iran zimefeli

#ParsToday. | Raisi: Njama za maadui za kuitenga Iran zimefeli

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia njama za karibuni za maadui za kutaka …

Alkhamisi tarehe 29 Septemba 2022

#ParsToday. | Alkhamisi tarehe 29 Septemba 2022

Leo ni Alkhamisi tarehe Pili Rabiul Awwal 1444 Hijria sawa na tarehe 29 Septemba 2022. …