Blinken awasili Afrika Kusini kituo cha  kwanza cha ziara yake ya mataifa matatu ya Afrika

#VOA. | Blinken awasili Afrika Kusini kituo cha kwanza cha ziara yake ya mataifa matatu ya Afrika

Mbali na Afrika Kusini, Blinken pia ataitembelea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda.

Blinken anatarajiwa kutoa hotuba muhimu nchini Afrika Kusini Jumatatu kuhusu mkakati wa Marekani kwa afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Mabadiliko ya hali ya hewa, biashara, afya na uhaba wa chakula vyote vitakuwa katika majadiliano.

Akiwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wanasema Blinken atafanya kazi ili kupunguza mivutano kati ya Congo na Rwanda. Congo imemshutumu jirani yake kwa kuliunga mkono kundi la waasi la M23, madai ambayo Kigali inakanusha.

Nchini Rwanda, Blinken atazungumzia “kufungwa kimakosa” kwa mkazi wa kudumu wa Marekani Paul Rusesabagina, kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje. Vitendo vya Rusesabagina vilisaidia kuwaokoa mamia ya watu wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 na kuhamasisha kutengenezwa filamu ya Hotel Rwanda.

Source link: Habari hii imetoka kwenye wavuti wa VOA Swahili.

About Habari za VOA

VOA - SAUTI YA AMERIKA: ni wakala wa media wa Merika ambao hutumika kama taasisi ya serikali ya Merika kwa utangazaji usio wa kijeshi, wa nje. Ni mtangazaji mkubwa zaidi wa kimataifa wa Merika. VOA inazalisha vitu vya dijiti, TV na redio katika lugha 47 ambazo husambaza kwa vituo vya ushirika kote ulimwenguni.

Check Also

Watu saba wafariki  kwa ugonjwa kipindupindu Haiti

#VOA. | Watu saba wafariki kwa ugonjwa kipindupindu Haiti

Haiti siku ya Jumapili imesema takriban watu saba wamefariki dunia kwa ugonjwa kipindupindu katika kurudi …

RDC : la Monusco note une amlioration de la situation des droits humains entre juin et septembre | Politico.cd

#PoliticoCD. | RDC : la Monusco note une amlioration de la situation des droits humains entre juin et septembre | Politico.cd

Dans un rapport adress au Conseil de Scurit de lONU, la Monusco note une nette …